Swali: Ni ipi hukumu ikiwa mtoto mwenye umri chini ya miaka mitano atapita mbele yetu wakati wa swalah? Ikiwa tukimzuia anaongeza kupita, hukaa mahali pa sujuud au juu ya kichwa cha anayeswali, khaswa akiwa chini ya miaka mitatu. Basi tufanye nini kwa mtoto wa namna hii?
Jibu: Ni wajibu kumzuia, kwa sababu ya ujumla wa dalili za Shari´ah juu ya hilo. Miongoni mwa dalili hizo ni maneno yake (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):
”Ikiwa mmoja wenu anaswali kuelekea kitu kinachomzuia watu kisha mtu akataka kupita mbele yake, basi amsukume. Akikataa basi apambane naye, kwani huyo ni shaytwaan.”
Ameipokea al-Bukhaariy na Muslim.
Maana ya maneno “apambane naye” ni kwamba amsukume kwa nguvu ili asipite mbele yake.
- Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (29/331)
- Imechapishwa: 13/03/2026
Swali: Ni ipi hukumu ikiwa mtoto mwenye umri chini ya miaka mitano atapita mbele yetu wakati wa swalah? Ikiwa tukimzuia anaongeza kupita, hukaa mahali pa sujuud au juu ya kichwa cha anayeswali, khaswa akiwa chini ya miaka mitatu. Basi tufanye nini kwa mtoto wa namna hii?
Jibu: Ni wajibu kumzuia, kwa sababu ya ujumla wa dalili za Shari´ah juu ya hilo. Miongoni mwa dalili hizo ni maneno yake (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):
”Ikiwa mmoja wenu anaswali kuelekea kitu kinachomzuia watu kisha mtu akataka kupita mbele yake, basi amsukume. Akikataa basi apambane naye, kwani huyo ni shaytwaan.”
Ameipokea al-Bukhaariy na Muslim.
Maana ya maneno “apambane naye” ni kwamba amsukume kwa nguvu ili asipite mbele yake.
Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
Tarjama: Firqatunnajia.com
Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (29/331)
Imechapishwa: 13/03/2026
https://firqatunnajia.com/mtoto-anataka-kupita-mbele-yangu-wakati-wa-swalah/