Swali: Vipi kuswali juu ya mto ambao umechongwa na misalaba?

Jibu: Kuhusu misalaba inatakiwa kufutwa. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alikuwa anapoona kitu chenye msalaba anauharibu. Hivo ndivo alivosema ´Aaishah. Msalaba huo unatakiwa kufutwa kwa kuweka kitu juu yake au kuharibu picha yake ili kisiwe na umbo la msalaba kwa njia ya kukata sehemu yake. ´Aaishah amesema:

“Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) hakuwahi kuona kitu kilicho na msalaba isipokuwa aliuteketeza.”

Kwa sababu picha ya msalaba ni yenye kuabudiwa badala ya Allaah.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/24124/حكم-الصلاة-على-وسادة-فيها-نقش-صلبان
  • Imechapishwa: 03/09/2024