Ibn Baaz kuhusu kwamba haifai kuzidisha katika kuosha mikono

Swali: Vipi ikiwa mtu atafanya kama Abu Hurayrah akazidisha katika kuosha mikono miwili?

Jibu: Kinachonidhihirikia ni kwamba ni Bid´ah, kwa sababu ni jambo ambalo halina msingi. Kule Swahabah kujitahidi jambo fulani haiwi ndio dalili. Ni kama kitendo cha Ibn ´Umar alipokuwa anataka ndevu zinazozidi ngumi na kuosha kwake macho yake mawili:

فَإِن تَنَازَعْتُمْ فِي شَيْءٍ فَرُدُّوهُ إِلَى اللَّـهِ وَالرَّسُولِ

”Mkizozana juu ya jambo, basi lirudisheni kwa Allaah na Mtume.”[1]

Hilo ni lenye kuenea. Isipokuwa yale yaliyopokelewa kutoka kwa makhaliyfah waongofu; ni sehemu ya Sunnah muda wa kuwa hayajapingana na Sunnah sahihi na iliyo wazi.

[1] 4:59

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/24123/حكم-المبالغة-في-غسل-اليدين-في-الوضوء
  • Imechapishwa: 03/09/2024