Swali: Inafaa kwangu kumuuzia ardhi mtu ambaye amechukua mkopo wa ribaa ili aweze kukinunua kiwanja hicho?
Jibu: Hapana. Haijuzu kumuuzia mtu ambaye analipa kwa pesa ya ribaa. Je, inafaa kwako kumuuzia bidhaa mtu ambaye ana pesa ya wizi ilihali na wewe unajua uhalisia wa pesa hiyo au amempokonya pesa hiyo mwenzie? Hapana, haijuzu kwako kufanya hivo. Hata hivyo inafaa ikiwa hujui ni wapi pesa yake imetoka. Lakini kama analipa kwa pesa unayojua kuwa ni ya haramu haijuzu kwako kumuuzia bidhaa hiyo.
- Muhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: Sharh ´Umdat-il-Fiqh (27)
- Imechapishwa: 13/04/2021
Mshirikishe mwenzako:
- Click to share on Telegram (Opens in new window) Telegram
- Click to share on WhatsApp (Opens in new window) WhatsApp
- Click to print (Opens in new window) Print
- Click to email a link to a friend (Opens in new window) Email
- Click to share on Facebook (Opens in new window) Facebook
- Click to share on X (Opens in new window) X
- Click to share on Pocket (Opens in new window) Pocket