Benki inakununulia ardhi baadaye wanakuuzia nayo

Swali: Ni ipi hukumu benki kuninunulia ardhi kisha wakaniuzia ardhi hiyo?

Jibu: Ikiwa benki watanunua ardhi, wakaimiliki na kubaki nayo, inafaa kwao wakakuuzia nayo. Lakini kitendo cha wao kukununulia nayo kisha ukalipa thamani yake na bei ya ziada, huo ni mkopo. Ziada unayolipa katika hali hiyo ni ribaa.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh ´Umdat-il-Fiqh (27)
  • Imechapishwa: 13/04/2021