Mswaliji kumuombea du´aa amtakaye kwenye Sujuud

Swali: Je, mtu kwenye Sujuud awaombee du´aa wazazi wake na watoto wake?

Jibu: Aombe kile kitachomuwepesikia. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Mja anakuwa karibu zaidi na Mola wake anapokuwa kwenye Sujuud. Hivyo basi, aombe du´aa kwa wingi.”

Ajiombee mwenyewe, wazazi wake, waislamu, waalimu zake, marafiki zake na wale waliomtendea wema.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/22635/حكم-الدعاء-في-السجود-للوالدين-والذرية
  • Imechapishwa: 14/07/2023