Mswaliji Haram hakuielekea Ka´bah ipasavyo

Swali: Baadhi ya waswaliji katika msikiti Mtakatifu hawaielekei Ka´bah ipasavyo licha ya kwamba wana uwezo wa kufanya hivo. Ni ipi hukumu ya swalah zao?

Jibu: Swalah zao ni batili. Kama wanaweza kuiona Ka´bah basi wanalazimika kuielekea ipasavyo. Serikali – Allaah awajaze kheri – wameweka alama ya misitari ya mwelekeo sahihi. Kwa hivyo mtu akielekea misitari hii inakuwa ni mwelekeo sahihi.

  • Muhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (12/412)
  • Imechapishwa: 01/05/2026