Msomaji Qur-aan anayepata thawabu mara mbili

Swali: Hadiyth ya ´Aaishah (Radhiya Allaahu ´anhaa) inayosema:

“Ambaye anasoma Qur-aan na inampa tabu… “

Jibu: Anapata thawabu mara mbili. Ina nini? Maana yake ni kwamba baadhi ya herufi zinampa tabu. Hata hivyo anajitahidi mpaka ajifunze. Hasemi kuwa hajui au si msomi. Anasoma, anajifunza, anasubiri, anawauliza ndugu zake na kadhalika. Mtu huyu anapata thawabu mara mbili; ujira wa kwanza ni kisomo na ujira mwingine ni wa kujitahidi.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/23409/معنى-الذي-يقرا-القران-وهو-عليه-شاق
  • Imechapishwa: 13/01/2024