Swali: Ni ipi hukumu ya kuswali nyuma ya Ibaadhiyyah?

Jibu: Enyi ndugu, sikilizeni! Msituletee mapote. Sisi tuko na kanuni: yule ambaye Bid´ah zake zinamtia kwenye ukafiri hakuswaliwi nyuma yake. Hili ni kwa makubaliano [ya wanachuoni wote]. Upande mwingine yule ambaye Bid´ah zake zinamtia kwenye ufusaki, hapa ndio wanachuoni wametofautiana. Kuhusu yule mwenye kufanya dhambi ndogondogo, huyu haina neno kuswali nyuma yake kwa kuwa sisi sote tuna dhambi ndogondogo. Ni wachache mno wanaosalimika na dhambi ndogondogo.

Je, kwa sasa mmejua kanuni hii? yule ambaye Bid´ah zake zinamtia kwenye ukafiri hakuswaliwi nyuma yake na swalah haisihi nyuma yake. Yule ambaye Bid´ah zake zinamtia kwenye ufusaki, [dhambi] ilio chini ya ukafiri, hapa ndio wanachuoni wametofautiana. Maoni sahihi ni kwamba kunaswaliwa nyuma yake kwa kuwa ni muislamu. Kuhusu yule mwenye dhambi ndogondogo kunaswaliwa nyuma yake pamoja na kuendelea kumnasihi pale ambapo kunadhihiri kitu katika dhambi hizo.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Kitaab Ahaadiyth-il-Fitnah http://www.alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/al_fitan%201-10-08-1433.mp3
  • Imechapishwa: 21/04/2015