Swali: Je, ni jambo limewekwa katika Shari´ah kufanya witiri katika mambo yote?

Jibu: Hili ndilo lililo karibu zaidi, isipokuwa katika yale ambayo Shari´ah imeeleza kuwa ni shufwa. Ndio maana Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alifanya hivo katika kula tende katika ´Iyd-ul-Fitwr. Alikuwa (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) akila tende witiri kabla ya kuswali swalah ya ´iyd. Allaah ameweka Shari´ah ya kufanya Twawaaf mara saba, Sa´y mara saba, kurusha vijiwe mara sana na kadhalika. Kwa hivyo msingi ni kwamba Witr inatakikana, isipokuwa katika kwa vile Shari´ah imeelekeza kuwa ni shufwa kama vile Rak´ah nne za Dhuhr, ´Aswr, ´Ishaa na Sunnah za Rak´ah mbilimbili.

  • Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/24456/هل-تستحب-مراعاة-الوتر-في-كل-الاشياء
  • Imechapishwa: 12/10/2024