95 – Tunaamini adhabu ya kaburi kwa yule mwenye kuiistahiki, maswali ya Munkar na Nakiyr ndani ya kaburi lake kuhusu Mola, dini na Mtume Wake, kutokana na vile ilivyopokelewa kutoka kwa Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) na Maswahabah zake (Radhiya Allaahu ´anhum).

MAELEZO

Bi maana katika makafiri na waislamu watenda madhambi. Wote wawili wametajwa waziwazi ndani ya Qur-aan. Vilevile yametiliwa nguvu na Hadiyth zilizopokelewa kwa wingi, kama alivosema Ibn Abiyl-´Izz na wengineo. Kwa hivyo ni wajibu kuyaamini. Lakini haijuzu kupekua namna yake, kwa sababu akili haiwezi kuelewa namna yake. Shari´ah haileti kitu ambacho hakifahamiki na akili, lakini wakati mwingine inaweza kuleta kitu ambacho inaifanya akili kuchanganyikiwa. Kwa hivyo ni wajibu kujisalimisha na jambo hilo. Unaweza kupata baadhi ya Hadiyth zilizoashiriwa katika maelezo ya Ibn Abiyl-´Izz na katika ”as-Sunnah”[1] ya Ibn Abiy ´Aaswim.

Maswali ya Munkar na Nakiyr ni jambo limepokelewa kwa wingi, isipokuwa kuwaita Malaika wawili hao ”Munkar” na ”Nakiyr” kumesimuliwa Hadiyth moja ambayo cheni yake ya wapokezi ni nzuri[2].

[1] Tazama ”Dhwilaal-ul-Jannah fiy Takhriyj-is-Sunnah” (863-877).

[2] Tazama “as-Swahiyhah” (1391).

  • Mhusika: Imaam Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-´Aqiydah at-Twahaawiyyah – Sharh wa Ta´liyq, uk. 84-85
  • Imechapishwa: 14/10/2024