Swali: Ni upi mfumo wa Ahl-us-Sunnah wal-Jamaa´ah na Salaf-us-Swaalih kwa wapiga visa? Je, ni jambo lililowekwa katika dini kutilia bidii kubwa visa vya ukweli?
Jibu: Qur-aan na Sunnah vinatosheleza. Tukisikia kisa sahihi kinachoafikiana na Qur-aan na Sunnah, ni sawa. Kuhusiana na visa vya kila siku, Salaf walitahadharisha juu ya wapiga visa kwa sababu kwa jumla ni kwamba wanasema uongo ili kutaka kuwaathiri watu. Kwa ajili hiyo wanataja vitu ili kuwaathiri watu hata kama itakuwa si sahihi. Hoja yao ni kuzitikisa nyoyo za watu. Si sawa. Allaah Ametutajia visa katika Qur-aan na Mtume Wake (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) ametutajia visa katika Sunnah. Ikiwa kisa kinafanana na vile vinavyopatikana katika Qur-aan na Sunnah, mtu akitaje.
- Muhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: Sharh Muqaddimati Ibn Abiy Zayd al-Qayrawaaniy fiyl-´Aqiydah (08) http://www.alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/mqirwani–14340317.mp3
Mshirikishe mwenzako:
- Click to share on Telegram (Opens in new window)
- Click to share on WhatsApp (Opens in new window)
- Click to print (Opens in new window)
- Click to email a link to a friend (Opens in new window)
- Click to share on Facebook (Opens in new window)
- Click to share on Twitter (Opens in new window)
- Click to share on Pocket (Opens in new window)