Swali: Watoto washike msimamo upi kwa baba yao ambaye anawaudhi sana kwa maneno na matendo?

Jibu: Wawe na subira kwake. Ni juu yao wawe na subira kwake na wamtendee wema. Huu ndio wajibu wao.

Pengine nyinyi ndio mnamkosea. Pengine nyinyi ndio mnamvulia adabu na matokeo yake ndio anawakulia mkavu kwa ukosefu wenu wa adabu na kuacha swalah na hamtaki kuambiwa lolote. Ikiwa hali ni namna hii basi nyinyi ni wenye kukosea na yeye ndiye mwenye kupatia.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: at-Tafsiyr al-Mufasswal (64) http://www.alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/tf–1432-04-02.mp3
  • Imechapishwa: 21/08/2020