Swali: Ni ipi hukumu ya kusema ”ni juu yangu haramu”?

Jibu: Ni sawa na kiapo. Akiona manufaa ya kwenda kinyume na kiapo chake basi atoe kafara. Isipokuwa ikiwa kama amekusudia kumharamisha mke wake, katika hali hiyo hukumu yake ni sawa na kumfananisha mke wake na mama yake. Katika hali hiyo atatoa kafara ya kumfananisha mke na mama. Lakini akisema ”ni juu yangu haramu kufanya kadhaa” au ”ni juu yangu haramu kumtembelea fulani”, makusudio yake ni kuizuia nafsi yake na hakukusudia kujiharamishia mke wake. Hukumu yake ni ya kiapo. Kama alivosema (Subhaanahu wa Ta´ala):

يَا أَيُّهَا النَّبِيُّ لِمَ تُحَرِّمُ مَا أَحَلَّ اللَّـهُ لَكَ ۖ تَبْتَغِي مَرْضَاتَ أَزْوَاجِكَ ۚ وَاللَّـهُ غَفُورٌ رَّحِيمٌ

“Ee Nabii! Kwanini unaharamisha kile alichokuhalalishia Allaah? Unataka kuwaridhisha wake zako na Allaah ni Mwingi wa kusamehe, Mwenye kurehemu.”[1]

[1] 66:01-02

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/24419/حكم-قول-علي-الحرام
  • Imechapishwa: 09/10/2024