Je, inafaa kufanya kile alichoapa kutokifanya kabla ya kutoa kafara?

Swali: Imepokelewa kwamba anatakiwa kutoa kafara kisha ndio afanye, au kwamba afanye kisha atoa kafara.

Jibu: Yamepokelewa yote mawili. Imekuja katika upokezi:

”Atoe kafara ya kiapo chake na afanye kile ambacho ni bora.”

Imekuja katika upokezi mwingine:

”Afanye kile ambacho ni bora na atoe kafara ya kiapo chake.”

Baadhi ya mapokezi yanasema:

”… kisha afanye kile ambacho ni bora.”

Atangulize kafara. Jambo ni lenye wasaa.

Kuhusu kafara ya kumfananisha mke wake na mama yake ni lazima kwanza atoe kafara:

فَتَحْرِيرُ رَقَبَةٍ مِّن قَبْلِ أَن يَتَمَاسَّا

”… ni kuacha huru mtumwa kabla ya kugusana.”[1]

Kuhusu kafara nyenginezo mbali na kafara ya kumfananisha mke wake na mama yake anayo khiyari. Hata hivyo akianza kutoa kafara ndio bora zaidi:

”Atoe kafara ya kiapo chake kisha afanye kile ambacho ni bora.”

[1] 58:03

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/24421/هل-يجوز-عمل-ما-حلف-عليه-قبل-الكفارة
  • Imechapishwa: 09/10/2024