Swali: Ni ipi kauli yenye nguvu juu ya mtu ambaye ni msafiri katika Ramadhaan akitoka katika mji wake na kwenda katika mji mwingine? Je, ale na kunywa ikiwa kama atakaa chini ya siku tatu au ajizuie kwa kuheshimu Ramadhaan?

Jibu: Akifikia katika mji ambao watu wake wamefunga na yeye akawa na rukhusa ya kula asile hadharani. Badala yake ale kwa siri sehemu ambapo sio hadharani kwa watu ili watu wasiwe na dhana mbaya kwake.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: http://www.alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/liqo%20%20-%2021%20-%2008%20-%201435.mp3
  • Imechapishwa: 09/04/2015