Msafiri amefupisha nyuma ya imamu mkazi anayeswali kwa kukamilisha

Swali: Swalah ya ´Ishaa ilinikuta nikiwa safarini ambapo nikaswali Rak´ah mbili nyuma ya imamu mkazi. Je, swalah yangu hiyo ni sahihi?

Jibu: Swalah yako si sahihi. Ni wajibu uirudie Rak´ah nne, kwa sababu imesihi kutoka kwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) yanayofahamisha kwamba msafiri akiswali nyuma ya mkazi, basi analazimika kuswali Rak´ah nne.

  • Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (30/215)
  • Imechapishwa: 15/03/2026