Mpangilio huu wa Answaar-us-Sunnah hauna asli katika Shari´ah

Swali: Sisi Sudan kuna kundi linalolingania katika ´Aqiydah ya Salaf na kundi hili linaweka mudiri mkuu na viongozi wengine mbalimbali na wanawalazimisha wanachama wao kumtii mudiri huyu katika mambo ya Ijtihaad…

Jibu: Mpangilio kama huu sijui kuwa una asli katika Shari´ah. Uongozi unakuwa kwa mtawala wa waislamu. Yeye ndiye anatakiwa kusikizwa na kutiiwa katika yaliyo mema na si katika maasi. Hili ni kosa kubwa kuwepo kundi lililokusanyika na kuita kiongozi ambaye wanamtii katika yale [yote] anayosema.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: http://sudansalaf.blogspot.no/2014/03/blog-post_9469.html
  • Imechapishwa: 30/08/2020