Mpaka al-Hallaaj alikuwa akisema kuwa ni muislamu

Ibn Baakuyaah amesema:

”Nilimsikia Ibn Khafiyf akiulizwa ni kipi anachoamini juu ya al-Hallaaj ambapo akajibu: ”Naonelea kuwa yeye ni mmoja katika waislamu.” Akaambiwa: ”Amekufurishwa na wanachuoni na sehemu kubwa ya waislamu.” Akasema: ”Ikiwa yale niliyoyaona kwake sio Tawhiyd, basi hakuna Tawhiyd katika dunia hii.”

Hili ni kosa kwa Ibn Khafiyf. al-Hallaaj wakati wa kuuliwa kwake alikuwa akimpwekesha Allaah na akipiga kelele kuwa Allaah yuko kwenye damu yake na kwamba yeye ni muislamu na akijitenga mbali na dini nyinginezo zote mbali na Uislamu, lakini hata zandiki hufanya hivo hadharani ingawa wanaficha uzandiki ndani ya miili yao. Wanafiki pia walikuwa wakitambua upwekekaji wa Allaah, wakiswali, wakifunga na wakiswali hadharani licha ya kuwa unafiki uko ndani ya mioyo yao.  al-Hallaaj hakuwa punda mpaka aoneshe uzandiki wake waziwazi mbele ya Ibn Khafiyf na wengineo, lakini alikuwa akiwaonyesha hayo wale wenye kuafikiana na uaminifu wake. Kuna uwezekano vilevile kwamba alikuwa zandiki katika kipindi fulani, akaacha dini, akadai uungu na akifanya shirki, kisha baadaye pindi alipoona kifo akasilimu na kurejea katika haki. Allaah ndiye anajua zaidi usiri wake. Lakini hata hivyo tunajitenga mbali kwa Allaah kutokamana na maneno yake, yalikuwa ni ukafiri mtupu. Alikuwa anaona kuwa Muumba amekita ndani ya baadhi ya watu watukufu – Allaah ametakasika kutokamana na hayo.

  • Mhusika: Imaam Shams-ud-Diyn Muhammad bin Ahmad adh-Dhahabiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Siyar A´laam-in-Nubalaa’ (14/351)
  • Imechapishwa: 31/10/2020