Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) baada ya kuamrisha kufuata Sunnah zake na Sunnah za makhaliyfah wake waongofu baada yake na akasisitiza kushikamana nazo barabara na kuziuma kwa magego, akasema:
“Tahadharini na mambo mepya.”
Bi maana ninakuonyeni na mambo ya kuzuliwa. Mambo ya kuzua yanayokusudiwa ni katika dini ya Allaah. Hilo ni kwa sababu asli ya mambo ambayo mtu anamuabudu kwayo Allaah na kujikurubisha Kwake ni kukomeka na uharamu mpaka kuwepo dalili juu ya kwamba jambo fulani limewekewa Shari´ah. Ndio maana Allaah (´Azza wa Jall) amewakemea wale wenye kuhalalisha na kuharamisha kwa matamanio yao. Amesema (Ta´ala):
وَلَا تَقُولُوا لِمَا تَصِفُ أَلْسِنَتُكُمُ الْكَذِبَ هَـٰذَا حَلَالٌ وَهَـٰذَا حَرَامٌ لِّتَفْتَرُوا عَلَى اللَّـهِ الْكَذِبَ
“Na wala msiseme zinazosifia ndimi zenu uongo: hii halali na hii haramu ili mumzulie Allaah uongo. Hakika wale wanaomzulia Allaah uongo hawafaulu. Ni starehe ndogo tu na watapata adhabu iumizayo.”[1]
أَمْ لَهُمْ شُرَكَاءُ شَرَعُوا لَهُم مِّنَ الدِّينِ مَا لَمْ يَأْذَن بِهِ اللَّـهُ
“Je, wanao washirika waliowaamuru dini yale ambayo Allaah hakuyatolea kwayo idhini?”[2]
قُلْ أَرَأَيْتُم مَّا أَنزَلَ اللَّـهُ لَكُم مِّن رِّزْقٍ فَجَعَلْتُم مِّنْهُ حَرَامًا وَحَلَالًا قُلْ آللَّـهُ أَذِنَ لَكُمْ ۖ أَمْ عَلَى اللَّـهِ تَفْتَرُونَ
“Sema: “Mnaonaje zile riziki alizokuteremshieni Allaah ambapo mkazifanya katika hizo ni haramu na halali. Sema: “Je, Allaah amekuidhinisheni au mnamzulia Allaah?”[3]
Kuhusiana na mambo ya kidesturi na mambo ya kidunia, hakemewi yule mwenye kuyazua. Isipokuwa ikiwa kama kuna andiko linaloonesha kuwa ni haramu au linaingia katika kanuni ya jumla ambayo inaonesha kuwa ni haramu. Kwa mfano magari, vipando na mfano wake hatusemi kuwa ni mambo ya kuzua haijuzu kuvitumia kwa kuwa hayakuwepo katika zama za Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Haya ni mambo ya kidunia. Kuhusiana na mavazi na mfano wake hatusemi usivae isipokuwa tu mavazi yaliyovaa Maswahabah. Vaa ukitakacho katika vile ambayo Allaah amekuhalalishia kwa sababu asli ni uhalali. Isipokuwa yale ambayo kuna andiko la Kishari´ah linalosema kuwa ni haramu kama mfano wa uharamu wa hariri kwa wanaume, dhahabu kwa wanaume, mavazi ya picha na mfano wa hayo.
[1] 16:116
[2] 42:21
[3] 10:59
- Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
- Mfasiri: Firqatunnajia.com
- Marejeo: Sharh Riyaadh-is-Swaalihiyn (02/284-285)
- Imechapishwa: 11/12/2024

Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
Mfasiri: Firqatunnajia.com
Marejeo: Sharh Riyaadh-is-Swaalihiyn (02/284-285)
Imechapishwa: 11/12/2024
https://firqatunnajia.com/mnasema-bidah-bidah-ndege-na-gari-pia-ni-bidah/
Mshirikishe mwenzako:
- Click to share on Telegram (Opens in new window)
- Click to share on WhatsApp (Opens in new window)
- Click to print (Opens in new window)
- Click to email a link to a friend (Opens in new window)
- Click to share on Facebook (Opens in new window)
- Click to share on Twitter (Opens in new window)
- Click to share on Pocket (Opens in new window)