Swali: Baadhi ya walinganizi wanaenda kwa mvuta sigara na wakati mwingine wanaweza hata kumpa pesa anunue sigara. Wanasema kwamba wanafanya hivo kwa ajili ya kulingania. Je, ni sahihi? Wanaketi nao wakati wanapotazama TV na wanasema kuwa eti mtu asiwakimbize watu kwa ajili ya kulingania. Je, kufanya hivi ni sahihi?

Jibu: Sio sahihi. Kukubali maovu ni uovu. Si sahihi kule kumpa kwake pesa anunue sigara. Badala yake anatakiwa kumnasihi na kumbainishia madhara ya maasi, ni mamoja maasi hayo ni sigara au mengine. Amtahadharishe nayo na ampe kwa mfano kaseti zinazoelekeza, vijitabu na vipeperushi. Namna hii ndivo mtu hufanya. Ama yeye mwenyewe kufanya maasi, kumnunulia sigara au akampa pesa anunue sigara sio sahihi.

Swali: Je, anapata dhambi?

Jibu: Bila shaka. Ambaye anashuhudia maovu anapata dhambi. Isipokuwa yule ambaye anahudhuria maeneo pa maasi kwa ajili ya kuyaondosha. Kwa mfano mtu akaketi na watu wanaotazama vipindi vya haramu na baada ya kitambo kidogo (na si papo kwa hapo ili waliwazike naye kwanza) kisha akawaeleza kwamba vitu hivyo ni haramu na haijuzu na akawanasihi. Wakiitikia na wakazima runinga, basi limefikiwa lengo, na wakiendelea basi atoke zake nje. Akiendelea kubaki baada ya hapo basi naye ni mwenye kupata dhambi.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Liqaa’ al-Baab al-Maftuuh (19 B)
  • Imechapishwa: 01/06/2021