Swali: Nina kipande cha ardhi ninacholima. Siku moja nilihitaji kiasi cha 10,000 SA ili nilipie deni nililokuwa nalo, kisha nikaweka ardhi rehani kwa 10,000 ambapo nikalipa deni lile nililokuwa nalo. Kisha ardhi hii ikabaki kwa yule mtu anaendelea kuilima na kunufaika na mazao yake yote mpaka nimlipe ile pesa. Je, katika hili kuna ribaa?
Jibu: Ndiyo, ribaa. Kitendo cha yeye anachukua ardhi, anailima na anafaidika nayo bila malipo kwa sababu ya kukupatia muda katika mkopo, mpaka umlipie mkopo, hili halijuzu. Hii ni ribaa, mkopo hauwi na ziada. Mkopo ni mfano kwa mfano bila ya ziada. Aa kumwekea sharti kwamba anafaidika na ardhi na kuitumia mpaka umlipie, basi hii ni kama umemkopesha 1,000 kwa 1,100 au kwa 1,200. Hii ni ribaa na haijuzu.
- Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/3419/حكم-استثمار-المرهون-حتى-سداد-القرض
- Imechapishwa: 27/08/2026
Swali: Nina kipande cha ardhi ninacholima. Siku moja nilihitaji kiasi cha 10,000 SA ili nilipie deni nililokuwa nalo, kisha nikaweka ardhi rehani kwa 10,000 ambapo nikalipa deni lile nililokuwa nalo. Kisha ardhi hii ikabaki kwa yule mtu anaendelea kuilima na kunufaika na mazao yake yote mpaka nimlipe ile pesa. Je, katika hili kuna ribaa?
Jibu: Ndiyo, ribaa. Kitendo cha yeye anachukua ardhi, anailima na anafaidika nayo bila malipo kwa sababu ya kukupatia muda katika mkopo, mpaka umlipie mkopo, hili halijuzu. Hii ni ribaa, mkopo hauwi na ziada. Mkopo ni mfano kwa mfano bila ya ziada. Aa kumwekea sharti kwamba anafaidika na ardhi na kuitumia mpaka umlipie, basi hii ni kama umemkopesha 1,000 kwa 1,100 au kwa 1,200. Hii ni ribaa na haijuzu.
Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
Tarjama: Firqatunnajia.com
Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/3419/حكم-استثمار-المرهون-حتى-سداد-القرض
Imechapishwa: 27/08/2026
https://firqatunnajia.com/mkopeshaji-ameshikilia-kiwanja-na-kukitumia-hadi-aliyekopeshwa-alipe-deni/