Mke mnaswara ambaye anadai kuwa amesilimu ila hatendei kazi Uislamu wake

Swali: Mke wa kaka yangu ni mnaswara. Amelinganiwa katika Uislamu mara nyingi bila ya mafanikio yoyote. Siku miongoni mwa siku akawaambia kuwa amesilimu. Lakini hawajaona kwake kinachojulisha juu ya Uislamu wake hata swalah haswali. Wakati alipoenda kwa familia yake wakamwambia kuwa bado yuko katika dini yake [ya kinaswara]. Vipi tutaamialiane naye?

Jibu. Taamilianeni naye kuwa sio muislamu na kuwa Uislamu wake haukuthibiti. Ataamiliwe kuwa bado ni mnaswara aliyebaki katika dini yake.

Check Also

Peleka mahakamani

Swali: Mimi nina dada anayegombana na mume wake mwenye madhehebu na mfumo wa Suufiyyah. Anampiga, …