Swali: Nina mume na nimesafiri kwenda hijjah bila ridhaa yake, naye anasema hatanikubalia. Nami ni mwanamke ninayependa hijjah. Ni ipi iliyo wajibu; kumtii mume au kufanya hijjah?

Jibu: Ikiwa hijjah ni ya faradhi, basi lililo wajibu ni kutekeleza amri ya Allaah (Subhaanahu wa Ta´ala). Unapaswa kufanya hajj ya faradhi ikiwa una uwezo, hata kama mume hakuridhia. Ama ikiwa ni hijjah ni ya kujitolea, basi haijuzu kwenda bila idhini yake. Usihiji isipokuwa kwa ruhusa yake, wala usisafiri bila idhini yake na wala usitoke nyumbani bila idhini yake. Kwa hajj ya faradhi, hapana, kwani utiifu ni katika mambo mema. Hakuna utiifu kwa kiumbe katika kumuasi Muumba. Ikiwa una uwezo, basi hiji.

  • Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (21/183)
  • Imechapishwa: 17/03/2026