Mali ya yatima inayozidi matumizi yake

Swali: Kuna yatima ambaye wazazi wake wamefariki. Tumemlea na kumlinda. Anao ami wawili, pia kuna watu wanaotaka kufanya kheri ambao wanampa mali. Wakati mwingine mali hiyo inachanganyika na mali yetu, huku tukijua kuwa kipato chetu ni kikubwa zaidi. Aidha tunamzingatia yatima huyo kama mmoja wa watoto wetu.

Jibu: Hapana vibaya kwenu katika kile anachopewa katika swadaqah, ikiwa ni sawa na matumizi mnayomfanyia au ni kidogo kuliko hayo. Ama kile kinachozidi juu ya matumizi yake, basi ni lazima mkihifadhi kwa ajili yake. Mnayo bishara njema ya kupata malipo makubwa kwa kumlea na kumfanyia wema.

  • Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (20/70)
  • Imechapishwa: 17/03/2026