Swali: Dada kutoka Amerika. Kuna wakati nachukua katika mali ya mume wangu pasi na yeye kujua, kiasi cha dola moja au mbili nazikusanya na kununua mahitajio ya watoto na ya nyumbani na kuzitumia katika biashara ndogo ambayo faida yake inarudi kwetu. Je, mimi ni mwenye madhambi kwa kufanya hivo?

Jibu; Mtake idhini mume wako, ewe binti yangu na wala usiitumie. Inaruhusu kwako kufanya hivyo pale ambapo mume wako atakuwa ni bakhili, anawabania wewe na watoto wako katika matumizi. Kutoka kwa Hind bint ´Utbah (Radhiya Allaahu ´anhaa) na ni mke wa Abu Sufyaan mama yake na Mu´aawiyah (Radhiya Allaahu ´anhum ajma´iyn), alisema: “Ewe Mtume wa Allaah! Abu Sufyaan ni mwanaume bakhili. Hatuhudumii mimi na watoto wangu kile kinachotutosheleza kwa wema isipokuwa mpaka nichukue kutoka kwenye mali yake ilihali na yeye hajui – yaani anachukua kwa ajili ya matumizi. Amesema (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):

“Chukua kile kitakachokutosheleza wewe na watoto wako kwa wema.”

Hivyo, ikiwa mume wako anakubania chukua matumizi tu. Na ikiwa hakubanii mtake kwanza idhini katika jambo hili na wala usichukue na ukaitumia pasi na kumuomba idhini kwanza.

  • Mhusika: Shaykh ´Ubayd bin ´Abdillaah al-Jaabiriy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: http://ar.miraath.net/fatwah/4351
  • Imechapishwa: 22/09/2020