Swali: Mimi ni mke na mume wangu ananikataza kutumia vidonge vya kuzuia mimba, kwani yeye hahisi uchovu ambao ninaupata. Mimi nimeathirika na nilimeza vidonge hivyo bila kumwambia mume wangu. Je, kuna dhambi katika hilo? Anafanya hivyo akisema: “Lea mtoto, vinginevyo utaweza kupata mimba.” Lakini nimekusudia kuacha vidonge hivyo baada ya hijjah. Je, nifanyeje?
Jibu: Ikiwa inawezekana kuyaacha, basi hilo ni bora zaidi. Hata hivyo ikiwa madhara yanakuwa makubwa na mzigo ni mkubwa, basi hapana vibaya katika kula vidonge hivyo ili kuepuka madhara. Lakini kwa ujumla bora ni kuacha kuvitumia. Kwa upande mwingine kumtii mume ni lazima, isipokuwa ikiwa inakuwa vigumu na kuna madhara kwako. Allaah (Subhaanahu wa Ta´ala):
فَاتَّقُوا اللَّـهَ مَا اسْتَطَعْتُمْ
”Mcheni Allaah muwezavyo.”[1]
[1] 64:16
- Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: Majmuu´-ul-Faatawaa (21/183)
- Imechapishwa: 17/03/2026
Swali: Mimi ni mke na mume wangu ananikataza kutumia vidonge vya kuzuia mimba, kwani yeye hahisi uchovu ambao ninaupata. Mimi nimeathirika na nilimeza vidonge hivyo bila kumwambia mume wangu. Je, kuna dhambi katika hilo? Anafanya hivyo akisema: “Lea mtoto, vinginevyo utaweza kupata mimba.” Lakini nimekusudia kuacha vidonge hivyo baada ya hijjah. Je, nifanyeje?
Jibu: Ikiwa inawezekana kuyaacha, basi hilo ni bora zaidi. Hata hivyo ikiwa madhara yanakuwa makubwa na mzigo ni mkubwa, basi hapana vibaya katika kula vidonge hivyo ili kuepuka madhara. Lakini kwa ujumla bora ni kuacha kuvitumia. Kwa upande mwingine kumtii mume ni lazima, isipokuwa ikiwa inakuwa vigumu na kuna madhara kwako. Allaah (Subhaanahu wa Ta´ala):
فَاتَّقُوا اللَّـهَ مَا اسْتَطَعْتُمْ
”Mcheni Allaah muwezavyo.”[1]
[1] 64:16
Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
Tarjama: Firqatunnajia.com
Marejeo: Majmuu´-ul-Faatawaa (21/183)
Imechapishwa: 17/03/2026
https://firqatunnajia.com/mke-anatumia-vidonge-vya-kuzuia-mimba-vila-mume-kujua/