Mke anampandishia sauti mume wake

Swali: Mke wake ana tabia mbaya na anampandishia sauti. Anapomnasihi anamjengea hoja kwa mke wa ´Umar bin al-Khattwaab (Radhiya Allaahu ´anh) ambaye alimpandishia sauti na kwamba kitendo hicho hakina neno. Je, dalili yake ni sahihi?

Jibu: Ndio. Amsubirie. Ikiwa anamtaka na ni mama wa watoto wake, amvumilie.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh ´Umdat-il-Fiqh (42)
  • Imechapishwa: 18/01/2024