Mke anaachika kutoka kwa mume aliyeshikwa na wazimu?

Swali: Mke anatalikika kutoka kwa mwanaume ambaye ameshikwa na wazimu?

Jibu: Hapana, mke wake hatalikiki kutoka kwake. Lakini mwanamke akiomba kufuta ndoa kwa ajili ya kujiondoshea madhara afanye hivo. Endapo atasubiri kwa sababu huenda fahamu ikamrudi au akamvumilia ni sawa vilevile.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Furqaan (10) http://alfawzan.af.org.sa/node/2053
  • Imechapishwa: 12/01/2017