Swali: Vipi mkao wa ihtibaa´ siku ya ijumaa?

Jibu: Maoni sahihi ni kwamba hapana vibaya. Hadiyth inayokataza mkao wa ihtibaa´ ni dhaifu. Baadhi ya Maswahabah wamefanya hivo. Lakini ikiwa kunasababisha usingizi au kitu katika uvivu mtu aache kufanya hivo. Wale wenye kuona kuwa inachukiza wamesema kuwa kunapelekea kulala na uvivu khaswa wakati wa Khutbah. Kinachopasa ni kusikiliza na kunyamaza.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/24266/حكم-جلسة-القرفصاء-يوم-الجمعة
  • Imechapishwa: 21/09/2024