Swali: Hadiyth inayokataza kuegemea?

Jibu: Hakuna makatazo. Kilichopo ni kwamba amesema kuwa yeye hali kwa kuegemea. Ameeleza kuwa yeye hali kwa kuegemea.

Swali: Kwa hiyo bora ni kuacha kufanya hivo?

Jibu: Hapana, hapati dhambi. Hata hivyo bora ni kuacha kufanya hivo kwa sababu Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema kuwa yeye hali kwa kuegemea. Hajasema msile. Alisema kwamba yeye ndiye hali. Inafahamisha kuwa kuacha hivo ndio bora na kwamba Sunnah ni kumuigiliza (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) katika jambo hilo.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/24267/حكم-الاتكاء-عند-الاكل
  • Imechapishwa: 21/09/2024