Swali: Baadhi ya watu wanapokatazwa kuvuta sigara, kunyoa ndevu au maasi mengine wanasema kuwa hayo ni mambo madogomadogo na matawi tu na kwamba sio wakati wake hivi sasa.

Jibu: Huyu ni mjinga wa kutupia. Afanyiwe ukali na kubainishiwa kwamba mambo ya dini hayaitwi namna hiyo kwamba ni ´maganda`. Mambo yote ya dini ni ya msingi, kheri na uongofu. Hilo ni kutokana na ujinga wake na uchache wa elimu yake.

Swali: Mtu huyo anajinasibisha na walinganizi?

Jibu: Haijalishi kitu. Awekewe wazi kwamba msemo huo ni khatari na kosa kubwa. Atubie na kumwomba Allaah msamaha.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/24009/حكم-من-يعد-الدخان-وحلق-اللحية-من-القشور
  • Imechapishwa: 15/08/2024