Swali: Kumsusa mwenye kuacha swalah baada ya kumnasihi?

Jibu: Ni jambo limewekwa katika Shari´ah kumkata. Ni jambo limewekwa katika Shari´ah. Bali ni jambo la wajibu kwa baadhi ya watu. Dogo liwezalo kusemwa ni kwamba ni jambo limewekwa katika Shari´ah. Isipokuwa ikiwa kama kufanya hivo kunasababisha shari zaidi. Katika hali hiyo litahitaji kuangaliwa vyema. Ususaji ni dawa na tiba; ikiwa kufanya hivo kunapelekea kheri basi mtu atafanya hivo, ikiwa kufanya hivo kunapelekea shari mtu atafanya hivo na ikiwa kutapelekea maovu zaidi basi mtu ataacha kufanya hivo mpaka wakati mwingine.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/24007/هل-يهجر-تارك-الصلاة-بعد-النصيحة
  • Imechapishwa: 15/08/2024