Swali: Tangu takriban siku tatu zilizopita kulitokea ugomvi kati yangu na mke wangu hadi siku hiyo nikawa na hasira kali sana isiyoweza kufikiriwa. Nikachukua kiatu – Allaah akuhifadhini – nikampiga mke wangu nacho. Nilipoteza fahamu kabisa, hali ya kuwa yeye ni mjamzito wa miezi sita na nina binti wa miaka miwili katika hali hizi ngumu. Mke wangu akaniambia nimtaliki na nilikuwa nimekasirika ambapo nikamwambia kuwa nimekutaliki, nimekutaliki, nimekutaliki. Nilirudia zaidi ya mara moja, lakini sijui idadi kamili, isipokuwa nina uhakika kabisa nilisema zaidi ya mara moja. Sasa niko katika hali ya kuchanganyikiwa, mke wangu analia nyumbani na hataki kuachana nami, na mimi pia vivyo hivyo. Nisaidieni nifanye nini, kwa sababu silali usiku?
Jibu: Hili ni kutokana na shaytwaan. Tunaomba Allaah atulinde sisi na nyinyi kutokana na shaytwaan. Ilikuwa ni wajibu kwako kujizuia na kutofanya haraka katika mambo na kujilinda kwa Allaah dhidi ya shaytwaan.
Hili linahitaji uje kwetu nyumbani kesho – Allaah akitaka – tutaliangalia jambo hili au siku ya jumamosi pia hakuna ubaya. Tutaliangalia suala hili pamoja na wewe au pamoja na mke na walii wake. Lazima kulitazama jambo hili na haitatokea isipokuwa kheri.
- Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/3342/حكم-الطلاق-باكثر-من-مرة-في-حالة-الغضب
- Imechapishwa: 15/08/2026
Swali: Tangu takriban siku tatu zilizopita kulitokea ugomvi kati yangu na mke wangu hadi siku hiyo nikawa na hasira kali sana isiyoweza kufikiriwa. Nikachukua kiatu – Allaah akuhifadhini – nikampiga mke wangu nacho. Nilipoteza fahamu kabisa, hali ya kuwa yeye ni mjamzito wa miezi sita na nina binti wa miaka miwili katika hali hizi ngumu. Mke wangu akaniambia nimtaliki na nilikuwa nimekasirika ambapo nikamwambia kuwa nimekutaliki, nimekutaliki, nimekutaliki. Nilirudia zaidi ya mara moja, lakini sijui idadi kamili, isipokuwa nina uhakika kabisa nilisema zaidi ya mara moja. Sasa niko katika hali ya kuchanganyikiwa, mke wangu analia nyumbani na hataki kuachana nami, na mimi pia vivyo hivyo. Nisaidieni nifanye nini, kwa sababu silali usiku?
Jibu: Hili ni kutokana na shaytwaan. Tunaomba Allaah atulinde sisi na nyinyi kutokana na shaytwaan. Ilikuwa ni wajibu kwako kujizuia na kutofanya haraka katika mambo na kujilinda kwa Allaah dhidi ya shaytwaan.
Hili linahitaji uje kwetu nyumbani kesho – Allaah akitaka – tutaliangalia jambo hili au siku ya jumamosi pia hakuna ubaya. Tutaliangalia suala hili pamoja na wewe au pamoja na mke na walii wake. Lazima kulitazama jambo hili na haitatokea isipokuwa kheri.
Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
Tarjama: Firqatunnajia.com
Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/3342/حكم-الطلاق-باكثر-من-مرة-في-حالة-الغضب
Imechapishwa: 15/08/2026
https://firqatunnajia.com/mje-nyumbani-nilitazame-suala-lenu/