Kuchana mwili wa maiti kwa ajili ya uchunguzi

Swali: Ni ipi hukumu ya kufanyia uchunguzi wa mwili wa maiti?

Jibu: Haijuzu kuchana maiti. Muislamu ana heshima. Kuvunja mfupa wake akiwa amekufa ni kama kuvunja akiwa hai. Si ruhusa kwa madaktari wala wengine kumchana. Lakini ikiwa kuna dharurah au haja, kama ametuhumiwa kwa jambo la uhalifu mkubwa wanataka kujua sababu zake au baadhi ya wahalifu wanajulikana ukweli wa makosa wanayotuhumiwa nayo, basi hilo halina ubaya kwa sababu ya haja. Ama kwa ajili ya kujifunza kwa kumfanyia muislamu, hilo halijuzu.

Swali: Lakini ikiwa familia yake wanakataa na yeye ni mtu aliyeuawa na familia yake hawataki kuchanwa kwake, lakini polisi wanasema lazima achanwe?

Jibu: Ikiwa kuna haja ya kiusalama – yaani usalama – na kukamata wahalifu, basi hakuna ubaya katika hilo. Ama kwa kusudi la kujifunza kwa wanafunzi, hapana. Lakini wajifunze kwa maiti zisizo na heshima, za makafiri wasiolindwa. Ama maiti za waislamu, hapana yeyote ajifunze juu yao, hazichanwi kwa sababu zina heshima.

Swali: Vipi maiti ya kafiri?

Jibu: Kafiri asiye na ulinzi hakuna ubaya.

  • Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/3347/حكم-تشريح-الميت
  • Imechapishwa: 15/08/2026