Swali: Nina mama na alikuwa na mtoto aliyefariki zamani. Sababu ya kifo ni kwamba alimfunika kwa shuka au blanketi na ilikuwa ya sufu na mtoto huyu alifariki kwa sababu ya blanketi hiyo. Pamoja na kuzingatia kwamba hakukusudia kufanya hivyo, bali ni kwa ujinga wake katika mambo kama haya. Je, anawajibika kulipa kafara?
Jibu: Ndiyo, ikiwa alimwekea mtoto blanketi nzito akafa kwa sababu hiyo, basi huku ni kuua. Lakini ni kuua kwa kukosea kwa sababu ya ujinga wake. Hivyo anawajibika kulipa fidia ya damu na kafara. Fiida ya damu, ikiwa baba yake au warithi watamsamehe, basi hakuna ubaya. Ama kafara, basi anawajibika kuacha huru mtumwa muumini, mwanamume au mwanamke. Ikiwa hawezi, basi afunge miezi miwili mfululizo, siku sitini, kwa sababu ya msiba huu uliotokea kutokana naye. Tunamuomba Allaah amsaidie na atusamehe sisi na yeye na waislamu.
Swali: Je, mama hawazuii warithi?
Jibu: Kwa hali yoyote, ikiwa baba yake yupo basi yeye ndiye anayerithi. Ikiwa kuna bibi anarithi, kwa sababu mama harithi kwa kuwa yeye ndiye aliyesababisha kifo. Ikiwa hana mtu isipokuwa jamaa wa ukoo wa kiume, basi hao ndio warithi.
- Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/3343/غطت-ولدها-بلحاف-فمات-هل-عليها-الدية-والكفارة
- Imechapishwa: 15/08/2026
Swali: Nina mama na alikuwa na mtoto aliyefariki zamani. Sababu ya kifo ni kwamba alimfunika kwa shuka au blanketi na ilikuwa ya sufu na mtoto huyu alifariki kwa sababu ya blanketi hiyo. Pamoja na kuzingatia kwamba hakukusudia kufanya hivyo, bali ni kwa ujinga wake katika mambo kama haya. Je, anawajibika kulipa kafara?
Jibu: Ndiyo, ikiwa alimwekea mtoto blanketi nzito akafa kwa sababu hiyo, basi huku ni kuua. Lakini ni kuua kwa kukosea kwa sababu ya ujinga wake. Hivyo anawajibika kulipa fidia ya damu na kafara. Fiida ya damu, ikiwa baba yake au warithi watamsamehe, basi hakuna ubaya. Ama kafara, basi anawajibika kuacha huru mtumwa muumini, mwanamume au mwanamke. Ikiwa hawezi, basi afunge miezi miwili mfululizo, siku sitini, kwa sababu ya msiba huu uliotokea kutokana naye. Tunamuomba Allaah amsaidie na atusamehe sisi na yeye na waislamu.
Swali: Je, mama hawazuii warithi?
Jibu: Kwa hali yoyote, ikiwa baba yake yupo basi yeye ndiye anayerithi. Ikiwa kuna bibi anarithi, kwa sababu mama harithi kwa kuwa yeye ndiye aliyesababisha kifo. Ikiwa hana mtu isipokuwa jamaa wa ukoo wa kiume, basi hao ndio warithi.
Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
Tarjama: Firqatunnajia.com
Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/3343/غطت-ولدها-بلحاف-فمات-هل-عليها-الدية-والكفارة
Imechapishwa: 15/08/2026
https://firqatunnajia.com/mama-amemuua-mtoto-wake-kwa-kumfunika-na-blanketi-nzito/