Mjane kumswalia mume wake msikitini wakati wa eda

Swali: Je, inafaa kwa mjane kwenda msikitini kwa ajili ya kuswalia mume wake swalah ya jeneza?

Jibu: Haina neno akafanya hivo mchana. Inafaa kwake kutoka nje kwa ajili ya mahitaji yake wakati wa mchana na sio usiku. Kumswalia mume wake swalah ya jeneza ni miongoni mwa haja.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh ´Umdat-il-Fiqh (40)
  • Imechapishwa: 06/05/2023