Swali: Ni vipi mtu anaweza kutofautisha kati ya usengenyaji na uvumi ambako unakutahadharisha na kuwasema vibaya na kutahadharisha Ahl-ul-Bid´ah wadh-Dhwalaal?

Jibu: Hili linategemea maslahi na nia. Ikiwa una uhakika kundi fulani ni Ahl-ul-Bid´ah na wanayoamini na ukatahadharisha nao, hii ni katika nasaha na sio usengenyaji wala uvumi. Hii ni nasaha. Lakini hata hivyo tatizo la leo ni kwamba hujui ni nini Bid´ah na watu wote ni watu wa Bid´ah kwa mujibu wako. Hivi watu wote wanatuhumiana Bid´ah. Wakati huo huo hawajui Bid´ah ni kitu gani. Inahusiana tu na mizozo ilio kwenye nafsi zao. Lilio la wajibu ni mtu asizungumze isipokuwa kwa elimu. Ni lazima kwa mtu azungumze kwa kiasi na haja tu na faida na asizidishe kuwasha moto juu ya mwingine.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Ighaathat-il-Lahfaan (30) http://www.alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/ighastah%20%20-%2025-12-1435.mp3
  • Imechapishwa: 16/06/2015