Mitume wengine wanapotajwa wanaswaliwa?

Swali: Je, kila anapotajwa Mtume au Nabii miongoni mwa Manabii aswaliwe kama jinsi anavyoswaliwa Mtume wetu Muhammad (Swalla Allaah ´alayhi wa sallam)?

Jibu: Ndio. Mitume wote wanaswaliwa (´alayhimus-Swalaatu was-Salaam). Vilevile hata kuwaswalia wasiokuwa Mitume katika baadhi ya nyakati ni sawa midhali hachukulii hilo kama alama fulani na ada. Lakini [kanuni inayojulikana ni kwamba] Mitume ndio wenye kuswaliwa, Maswahabah wanatakiwa radhi na waliokuja baada yao wanatakiwa rahmah.

  • Mhusika: ´Allaamah ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah ar-Raajhiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: http://subulsalam.com/play.php?catsmktba=4738
  • Imechapishwa: 01/05/2015