Swali: Baadhi ya watu walikuwa wakifundisha msikitini wakasema kwamba Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alikuwa akifanya baadhi ya madhambi madogo. Je, hili ni sahihi au si sahihi?

Jibu: Wanazuoni wamekhitalifiana kuhusu madhambi madogo kama yanatokea kwa Manabii au hapana. Kuna mitazamo miwili:

1 – Wanazuoni wengi wanaona kwamba yanaweza kutokea kwao madhambi madogo, lakini hawaachiwi juu yake. Bali huelekezwa na kuonywa na hivyo hawadumu nayo, bali huyaacha na hutubia kwa Allaah (Subhaanahu wa Ta´ala).

Ama madhambi makubwa, hayawatokei kabisa. Hivyo huenda yakatokea baadhi ya madhambi madogo, lakini hawaachiwi juu yake. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema kuhusu hilo:

اللهم اغفر لي ذنبي كله دقه وجله، وأوله وآخره، وعلانيته وسره، اللهم اغفر لي جدي وهزلي، وخطئي وعمدي، وكل ذلك عندي

“Ewe Allaah! Nisamehe madhambi yangu yote, madogo na makubwa, ya mwanzo na ya mwisho, ya wazi na ya siri. Ee Allaah! Nisamehe uzito wangu na mzaha wangu, makosa yangu na makusudi yangu na yote hayo yako kwangu.”

  • Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/3163/الاختلاف-في-وقوع-الانبياء-في-صغاىر-الذنوب
  • Imechapishwa: 26/07/2026