Amtii mama yake ambaye anamzuia kufunga swawm ya Sunnah?

Swali: Msichana anataka kufunga siku za jumatatu na alkhamisi, lakini mama yake anamzuia kwa hoja kwamba bado ni mdogo. Afanye nini? Je, amtii mama yake pamoja na kuwa ana uwezo wa kufunga?

Jibu: Ndiyo, swawm ya Sunnah ni jambo la kupendeza. Lakini kumtii mama ni wajibu. Mama anakusudia kheri, anakusudia kumhurumia na asijichoshe. Hata hivyo inampasa ashughulikie jambo hili kwa hekima, kwa maneno mazuri na kwa njia nzuri ili mama yake aridhie afunge ikiwa swawm haitamletea uzito wala madhara. Makusudio ni kwamba hili kutoka kwa mama linatokana na huruma na upendo. Kwa hivyo haifai kwa mchana kumuasi na kusababisha uovu baina yao. Bali ashughulikie jambo hili kwa maneno mazuri na mwenendo mwema pamoja na mama yake ili aridhie – Allaah akitaka – na aweze kufunga bila mashaka.

  • Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/3152/حكم-تقديم-صيام-التطوع-على-طاعة-الوالدة
  • Imechapishwa: 26/07/2026