Swali: Vipi ikiwa nadhiri ni kwa ajili ya kujikurubisha kwa Allaah?

Jibu: Ikiwa atanadhiri kwa ajili ya utiifu, basi inamlazimu kuitimiza. Mfano kama alivyosema Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):

“Yeyote atakayeweka nadhiri ya kumtii Allaah, basi na amtii.”

Ameipokea al-Bukhaariy katika ”as-Swahiyh” yake.

Kwa hiyo akisema ”Nimenadhiri kwa ajili ya Allaah nitatoa swadaqah ya pesa 100 kumpa fulani” au ”Pesa 1,000 kumpa fulani”, naye ana uwezo, basi inamlazimu. Au akasema ”Ni juu yangu kwa ajili ya Allaah kufunga siku ya alkhamisi”, ”Kufunga siku ya jumatatu” au ”Nitaswali Rak´ah mbili za Dhuhaa”, basi hilo linamlazimu.

Swali: Vipi ikiwa amekua na umri mkubwa na hawezi kufunga miaka miwili?

Jibu: Ikiwa ameshindwa kufunga, basi kufunga miaka miwili ni jambo lenye kuchukiza. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Hakufunga aliyefunga milele.”

Pale ´Abdullaah bin ´Amr alipotaka kufunga mwaka mzima, alimkataza. Akasema (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):

”Funga siku moja na acha siku moja.” Akasema: ”Ninaweza zaidi ya hilo.” Akasema: ”Hakuna bora kuliko hilo.”

Akamkataza kufunga mwaka mzima. Kufunga mwaka mzima ni jambo lenye kuchukiza, halifai. Hata aliweka nadhiri. Anachotakiwa ni kulipa kafara ya kiapo na hilo linatosha.

  • Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/1950/حكم-نذر-الطاعة
  • Imechapishwa: 26/07/2026