Kuna dharurah kwa vijana ya kufanya punyeto?

Swali: Nina mtoto wa kiume anayefanya sana kitendo cha kujitoa manii kwa mkono. Ni ipi hukumu yake? Je, inajuzu kufanya hivo kutokana na dharurah? Naomba jibu la kutosha na linalotuliza na Allaah akujaze kheri.

Jibu: Kitendo cha kujitoa manii kwa mkono ni jambo ovu na halijuzu. Hicho ndicho kinachoitwa punyeto na haijuzu. Kwa sababu kinapingana na maneno Yake Allaah (Subhaanahu wa Ta´ala):

وَالَّذِينَ هُمْ لِفُرُوجِهِمْ حَافِظُونَ إِلَّا عَلَىٰ أَزْوَاجِهِمْ أَوْ مَا مَلَكَتْ أَيْمَانُهُمْ فَإِنَّهُمْ غَيْرُ مَلُومِينَ فَمَنِ ابْتَغَىٰ وَرَاءَ ذَٰلِكَ فَأُولَـٰئِكَ هُمُ الْعَادُونَ

”Na wale ambao wanazihifadhi tupu zao, isipokuwa kwa wake zao au wale iliyowamiliki mikono yao ya kuume, basi hao si wenye kulaumiwa. Basi yeyote yule atakayetaka kinyume ya hivo, basi hao ndio wavukao mipaka.”[1]

Kwa hiyo mtu anayefanya kitendo hicho anatafuta njia nyingine isiyo halali ya kutoa manii nje ya ndoa. Kwa hiyo haijuzu kwake kufanya hivyo.

Kuna jambo jingine pia. Wanazuoni wa tiba wametaja kwamba kitendo hiki humdhuru mtu kwa madhara makubwa na kwamba kina athari mbaya zilizothibiti. Kwa sababu hiyo kinapaswa kuzuiwa kwa mambo mawili:

1 – Kwa dalili za Shari´ah.

2 – Kwa madhara yanayojulikana.

Kwa hiyo inamlazimu amche Allaah na ashughulikie matamanio yake kwa njia nyengine. Miongoni mwa njia hizo ni kufunga au kutumia baadhi ya dawa zinazopunguza nguvu ya matamanio. Ikiwa ana uwezo wa kuoa mke wa pili, wa tatu au wa nne, basi afanye hivyo. Aongeze wake ili uovu huo umwondokee.

[1] 23:05-07

  • Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/1946/ما-حكم-العادة-السرية-للحاجة
  • Imechapishwa: 26/07/2026