Swali: Ni ipi hukumu ya kuswali juu ya mikeka au mazulia yenye picha za wanyama, watu au mimea?

Jibu: Imechukizwa kuswali juu ya mikeka yenye maandishi au picha. Mambo hayo yanamshughulisha mwenye kuswali kutokamana na swalah yake. Hata hivyo swalah yake ni sahihi.

´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz

Swaalih al-Fawzaan

´Abul-´Aziyz Aal-ish-Shaykh

Bakr Abu Zayd

  • Mhusika: al-Lajnah ad-Daaimah
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Lajnah ad-Daaimah (05/378) nr. (17762)
  • Imechapishwa: 22/05/2022