Swali: Unasemaje juu ya watu wanaotoka kwa ajili ya kulingania kwa Allaah na wanaliwekea hilo kikomo kwa siku tatu na siku arobaini kwa lengo la kuwalingania watu katika Uislamu na kuwatengeneza watu?

Jibu: Kulingania kwa Allaah ni jambo linalotakikana. Lakini anayekuja na sharti zilizozuliwa hatuzikubali. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alilingania kwa Allaah na walinganizi baada ya Mtume walilingania kwa Allaah pasi na istilahi kama hizi, siku arobaini, miezi arobaini na mfano wake. Sharti hizi ni batili ambazo wamezizua wao wenyewe.

Kulingania kwa Allaah ni ´ibaadah. Haijuzu kuzua kitu kisichokuwa na dalili, Sunnah ya Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam).

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Liqaa’ Maftuuh bi ´Afiyf (59)
  • Imechapishwa: 22/05/2022