Miili ya watu wa Motoni

Swali: Je, ni kweli ya kwamba watu wa Motoni miili yao itafanywa kuwa mikubwa mpaka jino la mmoja wao liwe kubwa kama mlima wa Uhud?

Jibu: Ndio, hili limethibiti. Miili yao itafanywa kuwa mikubwa kiasi cha kwamba haiishi ili wapatwe kuadhibiwa vizuri na kupata maumivu – tunaomba kinga kwa Allaah.

لَا يَمُوتُ فِيهَا وَلَا يَحْيَىٰ

“Hatokufa humo na wala hatoishi.” (20:74)

Hawatokufa ili waweze kustarehe na wala hawatoishi maisha ya kutoepuka adhabu.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: at-Tafsiyr al-Mufasswal (09) http://www.alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/tf–1427-4-3.mp3
  • Imechapishwa: 19/08/2020