Swali: Je, inafaa kwetu kula kwenye migahawa ya USA ikiwa hatujui kama wamechinja kwa njia inayokubalika katika Shari´ah?
Jibu: Ikiwa ni katika watu wa Kitabu, mayahudi na manaswara, inafaa kula. Kwani Allaah amehalalisha kula chakula chao. Na kama ni katika vichinjwa vya waabudia mizimu, wakumonisti au wakanamungu, msizile. Tunachokusudia ni nyama. Ama chakula kama vile mchele na matunda vinaliwa kutoka kwa yeyote. Nyama katika migahawa ya mayahudi na manaswara ni halali. Ndio chakula chao na Allaah ametuhalalishia chakula chao.
- Muhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: Sharh ´Umdat-il-Fiqh (42)
- Imechapishwa: 07/01/2024
Mshirikishe mwenzako:
- Click to share on Telegram (Opens in new window)
- Click to share on WhatsApp (Opens in new window)
- Click to print (Opens in new window)
- Click to email a link to a friend (Opens in new window)
- Click to share on Facebook (Opens in new window)
- Click to share on Twitter (Opens in new window)
- Click to share on Pocket (Opens in new window)