Swali: Mwanamme anayeacha kumjamii mke wake zaidi ya miezi minne bila kuapa kwa Allaah ya kwamba hatofanya hivo. Je, hilo lina hukumu moja kama ya kuapa kwa Allaah kuwa hatomjamii (الإيلاء)?
Jibu: Ndio, ina hukumu moja kama ya kuapa kwa Allaah kuwa hatomjamii. Akiacha kumjamii mke wake zaidi ya miezi minne, basi ana hukumu moja kama ya mwenye kuapa kwa Allaah kuwa hatomjamii mke wake. Katika hali hii anatakiwa kutakwa kufanya hivo; atapewa khiyari ima amjamii au amtaliki. Afanye moja kati ya mawili ili kumuepushia madhara.
- Muhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: Sharh ´Umdat-il-Fiqh (38)
- Imechapishwa: 22/06/2023
Mshirikishe mwenzako:
- Click to share on Telegram (Opens in new window)
- Click to share on WhatsApp (Opens in new window)
- Click to print (Opens in new window)
- Click to email a link to a friend (Opens in new window)
- Click to share on Facebook (Opens in new window)
- Click to share on Twitter (Opens in new window)
- Click to share on Pocket (Opens in new window)