Swali: Mwanaume anataka kusafiri na akapiga kura kati ya wakeze ni nani ambaye ataenda naye. Hivyo kura ikamwangukia mmoja wao. Je, anatakiwa kupiga kura mara nyingine wakati ambapo atataka kusafiri?

Jibu: Dharurah. Anatakiwa kupiga kura kati yao katika kila safari. Yule ambaye kura itamwangukia ndiye atasafiri pamoja naye hata kama itamwangukia yuleyule ambaye alisafiri naye mara ya kwanza.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh ´Umdat-il-Fiqh (38)
  • Imechapishwa: 22/06/2023