Mgonjwa wa miaka mingi anataka kuchinja kwa ajili ya swadaqah

Swali: Mimi ni mtu nimefanyiwa uchawi kwa miaka mingi na Allaah hajaniandikia kupona mpaka hii leo pamoja na kwamba nafanya sababu za Kishari´ah. Je, inajuzu kwangu kuchinja kondoo kwa ajili ya Allaah (´Azza wa Jall) peke yake na kufanya Tawassul kumpwekesha kwangu katika ´ibaadah zangu na wakati huohuo kunuia aniponye tofauti na wanavofanya wachawi?

Jibu: Mosi ni kipi kimechokujuza kuwa maradhi ulio nayo ni uchawi? Maradhi ni mengi na hakuna mwenye kuyajua isipokuwa Allaah (Subhaanah). Sio lazima iwe ni uchawi.

Pili usikate tamaa ya kupona. Ni juu yako kuomba du´aa na kukithirisha kuleta nyuradi za asubuhi na jioni na Ruqyah ya Kishari´ah. Usikate tamaa Allaah atakuponya. Ukimtegemea Allaah na ukafanya sababu ikiwa ni pamoja na Ruqyah ya Kishari´ah kutoka kwa waja wema Allaah (Jalla wa ´Alaa) yukaribu Mwenye kujibu.

Kuhusiana na kuchinja haijuzu. Ukitaka kutoa swadaqah fanya hivo bila ya kuchinja. Toe swadaqah ya chakula, pesa, mavazi na vyengine pasi na kuchinja. Kwa sababu kuchinja ni jambo la khatari na kunakhofiwa pengine unachinja kwa sababu ya kuwatii makhurafi wanaokwambia uchinje ili uponywe. Hili halijuzu. Usichinje. Badala yake unaweza kununua nyama na ukawapa wahitaji. Ama kusema uchinje usifanye hivo.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Qaa´idah Jaliylah fiyt-Tawassul wal-Wasiylah (12) http://alfawzan.af.org.sa/node/2129
  • Imechapishwa: 05/07/2020